KARIBU

KARIBU SANA MTUMISHI WA MUNGU. KUNA MENGI YA KUJIFUNZA MAHALI HAPA. JISIKIE HURU KUTUMIA CHOCHOTE UTAKACHOKIPATA MAHALI HAPA. NA WEWE PIA UNAKARIBISHWA KUSHIRIKISHA WENGINE BARAKA MUNGU ALIZOKUPA. SHIRIKI PIA KATIKA KUSHAURI, KUONYA NA KUFUNDISHA ILI KANISA LA MUNGU YESU KRISTO LIZIDI KUSIMAMA. KARIBU SANA. KUMBUKA ENEO HILI HALIFUNGAMANI NA DHEHEBU LOLOTE BALI TUNAFUNGAMANA NA YESU KRISTO. BIBLIA NDIYO MAMLAKA KUU INAYOTUONGOZA KWA MAANA NDIYO NENO HALISI LA MUNGU.

Saturday, February 2, 2013

KARIBU CHRIST STUDIOS.
Unapoingia kwenye Blog hii kwa mara ya kwanza naomba ukutane na habari hii njema kwako. Kwa uzoefu wa miaka mingi nimefanya kazi ya kurekodi Mziki wa Injili na kwa neema ya Mungu nikapata kibali machoni pa watu wengi.
KWA NINI CHRIST STUDIOS?
Kwa wengi wanaonifahamu wangependa Studio iitwe kwa jina Langu ambalo wamelizoea. Lakini Studio hii si kwa ajili ya biashara tu bali mapato yake ni kwa ajili ya kueneza neno la Mungu. Nia na madhumuni yangu ni kwamba kutokana na ubora wa kazi tuzifanyazo, Kristo Yesu peke yake ndiye ainuliwa. Usipate shida wewe ukifika ARUSHA ulizia tu JOHN MTANGOO STUDIOS utafika.Lakini pia Lengo letu ni kuwapelekea vijana injili na hasa walioko Mashuleni  na Vyuoni. Ingependeza zaidi kwamba kila jambo jema juu yetu likinenwa basi kristo Yesu NDIYE ATAMKWE SANA!
WITO WETU.
Tunataka tuwe studio ya kisasa inayotoa kazi bora zenye kumtukuza Mungu.
MAONO YETU.
Maono yetu ni kuwafikia watu wengi kwa injili ya Yesu Kristo kupitia mziki.
KAZI TUZIFANYAZO.
Studio Yetu inafanya mlolongo wa kazi zifuatazo
- Kurekodi sauti (Audio Recording)
- Kurekodi Video (Video Recording)
- Kuandaa mziki (Music programming and arrangement).
- Kufundisha Sauti (Vocal Training).
- Shule ya mziki
- Kurekodi Mtangazo ya Biashara
- Kurekodi mahubiri
- Kuandaa vipindi vya redio
KAZI TULIZOFANYA.
Mungu ametupa Neema ya kuhudumu na vikundi vingi sana. Baadhi vimefanikiwa sana. Miongoni mwa waliofanikiwa baada ya kufanya kazi na sisi ni
- BEATRICE MUHONE (Ingoje Ahadi & Si njia Rahisi)
- JACKSON BENT (Si njia rahisi)
- MIRIAM lukindo (Asubuhi)
- TUMAINI (Shangilieni) KWAYA (Unishike & Nyimbo za matumaini) pamoja na LIVE RECORDING ya nyimbo za matumaini.
- MAMAJUSI KWAYA MOSHI - Majira ya jioni
- GODWIN OMBENI - Huyu Album zake zote pamoja na mpya ya Band yake amefanyia kwetu.
- IMANI KWAYA KKKT - KIPAWA Dar - es - salaam -- Hawa pia wamefanya na sisi Album zao za mwisho mbili. Usishangae kwamba tunapata na vikundi kutoka DAR, maana tumefanya kazi na kwaya nyingi sana Tanzania na Kenya.
MOBILE STUDIO
Dunia inaenda kasi sana. Maisha yamekuwa magumu na upatikanaji wa pesa ni changamoto isiyo na majabu. Kwa kutambua hili tuna studio inayokufuata mahali ulipo. Haijalishi ni kwaya ama mtu binafsi wewe tuambie tu na tutakufikia.

Kwa maelekezo zaidi tafadhali usisite kututebelea.
Tunapatikana
ARUSHA - Nanenane (njiro)
+255787416177 na +255766159501
Email:johnmtangoo@gmail.com



No comments:

Post a Comment