KARIBU

KARIBU SANA MTUMISHI WA MUNGU. KUNA MENGI YA KUJIFUNZA MAHALI HAPA. JISIKIE HURU KUTUMIA CHOCHOTE UTAKACHOKIPATA MAHALI HAPA. NA WEWE PIA UNAKARIBISHWA KUSHIRIKISHA WENGINE BARAKA MUNGU ALIZOKUPA. SHIRIKI PIA KATIKA KUSHAURI, KUONYA NA KUFUNDISHA ILI KANISA LA MUNGU YESU KRISTO LIZIDI KUSIMAMA. KARIBU SANA. KUMBUKA ENEO HILI HALIFUNGAMANI NA DHEHEBU LOLOTE BALI TUNAFUNGAMANA NA YESU KRISTO. BIBLIA NDIYO MAMLAKA KUU INAYOTUONGOZA KWA MAANA NDIYO NENO HALISI LA MUNGU.

Monday, April 1, 2013

IBADA YA UMOJA WA MAKANISA ARUSHA - MFANO WA KUIGWA



Kwa muda mrefu umoja wa madhehebu Arusha umekuwa ni mfano wa kuigwa. Ibada hii ya pamoja ya ijumaa kuu imedumu kwa miaka mingi. Kila wakati kama huu tofauti zote za kidhehebu huwekwa kando na kushuhudia umoja wa kipekee baina ya wachungaji na mapadri. Maaskofu wa makanisa mbalimbali hupata muda wa kutoa nasaa kwa waamini wao. Viongozi wa kisiasa hupata nafasi ya kusalimia wapiga kura wao. kwa hakika huu umoja unapaswa kudumishwa. Kama kawaida kitu chochote kizuri huwa hakikosi changamoto. Blog hii inapenda kutoa changamoto zifuatazo.
1. Kwa nini Umoja wa madhehebu ya kikristo Arusha hauna maono ya kununua vyombo vya mziki? kwa hakika kama kila mchungaji(kanisa) angechangia angalau 500,000 kwa mwaka naamini vingepatikana vyombo bora sana vya mziki. Kwa miaka nenda rudi changamoto ya vyombo vya mziki (PA) imekuwa sugu. wengi wa waamini ambao hawapo karibu na jukwaa kuu huwa hawapati mawasiliano vyema. Baba zetu hebu liangalieni hili.
2. Jukwaa. Kwa hali ya uwanja wowote wa mpira jukwaa kuu huwa halileti picha ya muunganiko kwa wasikilizaji. Ni vema jukwaa kuu likawekwa angalau katikati ya uwanja. Kwa nguvu ya umoja huu mkitushirikisha waamini wenu jamani hatushindwi kuchonga jukwaa bora na kubwa litakalohudumia ibada hii kwa namna ya kipekee.
3. Nyakati za nyuma tulizoea kuwa na mikutano ya injili inayohudumiwa na umoja wa madhehebu ya kikristo Arusha. Tafadhali fufueni enzi hizo ambako mikutano haikuwa kwa ajili ya kukua kwa dhehebu fulani bali kuuleta pamoja mwili wa kristo.
Je? wewe mmwenzangu una maoni gani ili umoja huu uzidi kusonga mbele?
Karibu utoe maoni yako na wewe!

No comments:

Post a Comment